Psalms 114

Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri


1 aWakati Israeli walipotoka Misri,
nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

2 bYuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,
Israeli akawa milki yake.


3 cBahari ilitazama ikakimbia,
Yordani ulirudi nyuma,

4 dmilima ilirukaruka kama kondoo dume,
vilima kama wana-kondoo.


5 eEe bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,
nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,

6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,
enyi vilima, kama wana-kondoo?


7 fEe dunia, tetemeka mbele za Bwana,
mbele za Mungu wa Yakobo,

8 galiyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,
mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.
Copyright information for SwhKC